Asilimia 79.17 ya wanafunzi Shule za Kanisa Katoliki wamefaulu kidato cha IV 2018

Baada ya Baraza la mitihani kutangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018  huku shule za Kanisa Katoliki zikiongoza kwa ufaulu, imebainishwa kuwa, Asilimia 79.17 ya wanafunzi shule za Kanisa Katoliki wamefaulu.

Mkuu wa Idara ya Elimu Baraza la maaskofu katoliki Tanzania TEC Padri Alphonce Raraiya  amebainisha kuwa, Jumla ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne kitaifa ni 356,869 sawa na asilimia 100%

Jumla ya wanafunzi waliofaulu ni 282,568 sawa na asilimia 79.17%

Jumla ya wanafunzi waliofeli ni 74,301 sawa na asilimia 20.82%

Jumla ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2018 kutoka katika shule zinazomilikiwa na kuendeshwa na Kanisa Katoliki Tanzania ni 19,738 sawa na asilimia 5.53%

Jumla ya wanafunzi waliofaulu katika shule za Kanisa Katoliki ni 19,293 sawa na asilimia 6.82%

Jumla ya wanafunzi waliofeli katika shule za Kanisa Katoliki ni 272 sawa na asilimia 0.36%

Kitaifa waliofaulu Daraja la kwanza ni     13,524.

                                Daraja la pili        ni      38,107.

                                Daraja la tatu       ni      60,636.

                                Daraja la nne        ni   170,301.

                                Waliofeli                ni      74,301         

Kadiri ya idadi ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2018 kutoka katika shule za Kanisa Katoliki;

Jumla ya wanafunzi waliofaulu  Daraja la kwanza ni  5,384sawa na asilimia 39.81%

                                                    Daraja la pili ni         6,813 sawa na asilimia   17.87%

                                                    Daraja la tatu ni         4,444 sawa na asilimia   7.32%

                                                    Daraja la nne ni         2,863 sawa na asilimia   1.68%

  Jumla ya wanafunzi waliofeli ni    272 sawa na asilimia    0.36%

 

Upembuzi wa matokeo ya mtihani wa kidateo cha nne kwa mwaka 2018 yanaonesha kushuka kidogo karibu kwa nukta mbili asilimia. Mwaka 2017 tulikuwa na asilimia sita nukta kumi (6.10%) ya ufaulu kati ya asilimia sabini na saba nukta tano saba (77.57%) ya ufaulu kitaifa. Mwaka 2018 tuna asilimia sita nukta nane mbili (6.82%) kati ya sabini na tisa nukta moja saba (79.17) ya ufaulu kitaifa.

Hongereni sana walimu kwa jitihada mnazofanya kuondoa ujinga katika vichwa vya vijana wetu. Hongereni sana shule zinazojitahidi kila uchao kufanya vizuri kimasomo na kuwajenga kimaadili. 

Wito kwa walimu wetu wafanye kazi kwa bidii zaidi kuwasaidia wanafunzi wetu waweze kufaulu vizuri zaidi.

Upembuzi wa matokeo haya umsaidie Mwalimu Mkuu, Mwalimu wa Taaluma pamoja na walimu wengine kuona, kutafuta ushauri na kujifunza kutoka katika shule zinazofaulu vizuri.

 

Tazama matokeo hapa